Rais Samia: Tunatekeleza Ilani kwa vitendo

HomeKitaifa

Rais Samia: Tunatekeleza Ilani kwa vitendo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu amesema serikali yake ya awamu ya sita inafanya kazi kwa kuzingatia maagaizo yaliyotolewa na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwani ndio ramani ya kuwatumikia na kuwapatia wananchi maendeleo na kutatua changamoto zao.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la Msingi la mradi wa maji wa Mtyangimbole, Madaba mkoani Ruvuma tarehe 24 Septemba, 2024.

Amesema hayo alipokuwa akiweka Jiwe la Msingi la mradi wa maji wa Mtyangimbole, Madaba mkoani Ruvuma tarehe 24 Septemba, 2024.

“Wakati wa Kampeni tuliahidi kumtua mama ndoo kichwani sasa tumekwenda kuifanyia kazi ahadi ile. Tumeifanyia kazi kwa kusambaza miradi ya maji nchi nzima. Kama mnavyoona tulivyofanya Ruvuma na nchi nzima ni hivyo hivyo.” amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia amesema ifikapo mwaka 2025 vijiji vyote vya Tanzania vitakuwa vimefikiwa na majisafi na salama kwa asilimia 85 na asilimia 95 kwa upande wa miji kama ambavyo ilani inaelekeza.

error: Content is protected !!