Rais Samia awapatia gari wanafunzi wa Shule ya Samia Namtumbo

HomeKitaifa

Rais Samia awapatia gari wanafunzi wa Shule ya Samia Namtumbo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekubali ombi la kuwapatia gari la shule wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyopo wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma.

Ombi lilitolewa na Dada Mkuu wa Shule hiyo, Stella Magaho alipokuwa akitoa neno la shukrani kwa Rais Samia kwa kuwajengea shule hiyo.

“Wakati Rais wa wanafunzi anazungumza aliomba gari la shule, aya sasa gari lipo njiani linakuja.”amesema Rais Samia.

Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyopo wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma.

Leo ikiwa ni siku yake ya tano ya ziara mkoani Ruvuma, Rais Samia ameizindua rasmi shule hiyo ya wasichana iliyogharimu kiasi cha shilingi bilioni 4.643 na uwezo wa kuchukua zaidi ya wanafunzi 1000 kwa mkupuo

error: Content is protected !!