Mzee: hakuna haja kuandikwa katiba mpya

HomeKitaifa

Mzee: hakuna haja kuandikwa katiba mpya

Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Abdulhamid Yahya Mzee amesema hakuna haja ya kuandikwa katiba mpya na badala yake iliyopo ifanyiwe marekebisho katika vipengele vinavyodaiwa kuwa na utata.

Aliyasema hayo wakati akiwasilisha maoni yake kwa kikosi kazi cha ukusanyaji maoni kuhusu masuala ya demokrasia kilichoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

“Mimi maoni yangu kwa ujumla mchakato uendelee pale ulipoishia lakini pale ambapo kuna vipengele ambavyo vilileta mvutano vifanyiwe marekebisho na zaidi vipelekwe kwa wananchi ili waweze kuvijadili,” alisema Mzee.

Alisema hakuna haja ya kuanza upya mchakato wa Katiba lakini ni muhimu wananchi wapewe fursa ya kutoa maoni kama kuna kasoro au changamoto.

Mzee alisema hana tatizo kuhusu muundo wowote wa Muungano kama ni wa serikali moja, mbili au tatu, cha msingi ni kuzingatia fursa sawa baina ya pande mbili, yaani Zanzibar na Tanzania bara.

error: Content is protected !!