JESHI la Polisi limefafanua kuwa linaendelea na ufuatiliaji wa tukio la kupotea kwa Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, Abdul Nondo.
Taarifa iliyotolewa leo na msemaji wa jeshi hilo, David Misime imeeleza kuwa saa 11 alfajiri ya leo katika eneo la Mbezi Luis, stendi ya mabasi ya Magufuli mwanaume mmoja alikamatwa kwa nguvu na watu waliotumia gari lenye namba za usajili T 249 CMV Land Cruiser nyeupe.
“Ilielezwa na mashuhuda kuwa katika purukushani za ukamataji begi dogo lilidondoshwa na baadhi ya vitu vilivyokuwemo vimetambuliwa vya Abdul Omary Nondo,” imeeleza taarifa hiyo.