Rais Samia: Kwaheri Dkt. Ndugulile

HomeKitaifa

Rais Samia: Kwaheri Dkt. Ndugulile

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaongoza waombolezaji kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirala la Afya Duniani (WHO) Marehemu Faustine Engelbert Ndugulile katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waombolezaji, Rais Samia ametoa pole kwa ndugu, jamaa, marafiki na watanzania kwa ujumla kufuatia kifo cha Dkt. Ndugulile na kueleza kama kiongozi wa nchi anamshukuru Mungu kwa zawadi ya uhai ya Dkt. Ndugulile.

Rais Samia akiwafariji wanafamilia wa aliyekuwa Mbuge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Dunia (WHO) Kanda ya Afrika, Dkt. Faustine Ndugulile.

Aidha, Rais Samia amesema Tanzania itaingia tena kwenye kinyang’anyiro kuipata nafasi aliyofanikiwa kuipata Marehemu Dkt. Ndugulile ya Ukurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika, ili kuendelea kutunza heshima iliyopata nchi.

Rais Samia akitoa heshima za mwisho kwenye jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mbuge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Dunia (WHO) Kanda ya Afrika, Dkt. Faustine Ndugulile.

error: Content is protected !!