Rais Samia apanda viwango Forbes

HomeKimataifa

Rais Samia apanda viwango Forbes

Jarida la Forbes la nchini Marekani limemtaja Rais Samia Suluhu Hassan kuwa miongoni mwa wanawake 100 wenye nguvu zaidi duniani akishika nafasi ya 91 kutokana nafasi ya 93 mwaka jana.

Hii mara ya nne jarida la Forbes kumuweka Rais Samia katika orodha hii huku sababu kuu ikiwa ni namna ambavyo aliweza kupambana dhidi ya ugonjwa wa Uviko-19 nchini Tanzania.

Wasifu wa Rais Samia uliowekwa katika mtandao wa Forbes umeeleza kwa muhtasari na kumtambua kama Rais wa awamu ya sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa kwanza mwanamke Tanzania. Forbes wameongeza pia, mnamo mwezi Septemba mwaka 2021 Rais Samia amekuwa mwanamke wa tano kutoka barani Afrika kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambapo aliweza kuzungumzia usawa katika upatikanaji na ugawaji wa chanjo za Uviko-19 duniani.

Aidha, Forbes wameeleza kuwa Rais Samia amejipambanua na kujitofautisha na mtangulizi wake, ambapo yeye amekuwa muumini mzuri wa sheria na taratibu zinazowekwa na Jumuiya za Kimataifa katika kupambana na Uviko-19, ikiwemo kuruhusu chanjo, karantini kwa wageni waingiao Tanzania na uhimizaji wa matumizi ya barakoa.

error: Content is protected !!