Rais Samia Suluhu kuongoza Mkutano wa kujadili mgogoro wa DRC

HomeKitaifa

Rais Samia Suluhu kuongoza Mkutano wa kujadili mgogoro wa DRC

Dar es Salaam – Rais wa Kenya, William Ruto, amethibitisha kuwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Félix Tshisekedi, na Rais wa Rwanda, Paul Kagame, watahudhuria mkutano wa dharura utakaofanyika Tanzania wikiendi hii kujadili mgogoro unaoendelea katika eneo la Mashariki mwa DRC.

Mkutano huo utafanyika Dar es Salaam siku ya Jumamosi, ukihusisha viongozi wakuu wa Afrika, wakiwemo Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, na Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud. Hafla hiyo itaongozwa na mwenyeji wake, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, na itaanza siku ya Ijumaa kwa mazungumzo ya mawaziri kabla ya mkutano wa wakuu wa nchi siku ya Jumamosi.

Mkutano huu unakuja wakati hofu ikiongezeka kuhusu mafanikio ya waasi wa M23 mashariki mwa DRC, kundi linalodaiwa kuungwa mkono na Rwanda, pamoja na mvutano wa kidiplomasia kati ya mataifa kadhaa ya Afrika. Mazungumzo yanatarajiwa kujikita katika juhudi za kurejesha amani na utulivu katika eneo hilo, ambalo limekuwa likishuhudia ongezeko la machafuko na watu kupoteza makazi yao.

error: Content is protected !!