Balozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mhe. Said Mshana amempokea Waziri Mkuu wa DRC, Mhe. Judith Suminwa aliyewasili nchini Tanzania alfajiri ya Februari 8, 2025 kushiriki Mkutano wa Dharura wa Pamoja Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika hapo baadaye.
Jumuiya zote mbili zinakutana kujadili kwa lengo la kupatia ufumbuzi hali ya ulinzi na usalama katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.