Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabid Kombo (Mb.), tarehe 21 Februari, 2025 jijini Budapest, Hungary, amekutana kwa mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Hungary, Mhe. Péter Szijjártó.
Pamoja na mambo mengine, Mhe. Kombo ameishukuru Serikali ya Hungary kwa uamuzi wa kufungua ofisi ndogo ya ubalozi nchini Tanzania utakaosaidia kuimaridha ushirikiano zaidi baina ya Tanzania na Hungary.
Waziri Szijjártó amesema Hungary inaoanga kufungua ofisi hiyo ndogo ya ubalozi Septemba mwaka huu.
Kufuatia kuimarika kwa ushirikiano baina ya Tanzania na Hungary na mwaliko kutoka Serikali ya Tanzania, Hungary imeridhia kufungua Ubalozi Mdogo jijini Dar Es Salaam utakaosaidia kuimarisha zaidi ushirikiano na Tanzania. Akizungumza hayo, Mhe. Waziri Szijjártó amebainisha kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi za kipaumbele barani Afrika kwa Hungary.
Aidha, Mhe. Waziri Szijjártó ameahidi kuwa kwa kutambua umuhimu wa ushirikiano wa Tanzania na Hungary, atafanya ziara nchini mwezi Septemba mwaka huu ikiwa pia ni pamoja n kuzindua Ofisi hiyo ambayo ujenzi wake utaanza mapema iwezekanavyo na unatarajiwa kukamilika mapema mwezi Septemba mwaka huu.
Kwa sasa nchi ya Hungary inawakilishwa nchini kupitia ubalozi wake uliopo Naorobi, Kenya.