Rais Samia apendekeza shule iitwe Beatrice Shelukindo

HomeKitaifa

Rais Samia apendekeza shule iitwe Beatrice Shelukindo

RAIS Samia Suluhu Hassan ameomba Shule ya Sayansi ya Wasichana ya Mkoa wa Tanga iliyopo Wilaya ya Kilindi aliiyoizinduliwa leo ipewe jina la aliyewahikuwa mbunge wa jimbo hilo Beatrice Shelukindo ili kuenzi upambanaji wake kwa maendeleo ya jimbo hilo.

Beatrice Shelukindo alifariki dunia March 2021, akiwa mbunge wa jimbo hilo.

Rais Samia ametoa rai hiyo kwa Mkuu wa Mkoa huo, Dk Batrida Buriani baada ya shule hiyo kutopewa jina mpaka sasa na kutumia jina la mkoa.

“Namimi nataka kuomba mkubali ombi langu Kilindi hapa tulikuwa na mpambanaji wa mambo ya kike najua leo angesikia furaha na faraja kubwa saana kwamba shule hii imejengwa hapa kwao ni Beatrice Shelukindo, kwa hiyo nikuombe Mkuu wa Mkoa ikiwapendeza mnaweza kuzingatia jina hilo”.

Shule hiyo inayojengwa kwa awamu mbili, ambapo awamu ya imejumuisha mabweni manane, bwalo la chakula, jengo la utwala, madarasa 12 ya kidato cha kwanza hadi nne, maabara, na nyumba za walimu 2 pamoja na zahanati.

Katika awamu ya pili, nyumba tatau za walimu zinatarajiwa kuongezwa kufanya jumla ya nyumaba tano ,mabweni matano kukamilisha mabweni 12.

Kwa upande wake, Mbunge wa Kilindi Omari Kigua amesema wamepokea Sh bilioni 13 kwa ajili ya shule pekee, shule za sekondari za juu ‘A level’ ziko nne, na hivi karibuni wilaya hiyo inatarajiwa kupokea shule zingine 4 na kufanya wilaya hiyo kuwa na shule 8 za elimu ya sekondari ya juu.

error: Content is protected !!