Tanzania kuiwekea vikwazo Afrika Kusini na Malawi kuhusu biashara ya bidhaa za kilimo

HomeKimataifa

Tanzania kuiwekea vikwazo Afrika Kusini na Malawi kuhusu biashara ya bidhaa za kilimo

Waziri wa Kilimo wa Tanzania, Hussein Bashe, ametangaza kuwa Tanzania itazuia uingizwaji wa mazao na bidhaa zote za kilimo kutoka Malawi na Afrika Kusini kuanzia Jumatano ijayo, iwapo nchi hizo hazitafungua masoko yao kwa bidhaa za Kitanzania kama ndizi, unga, mchele, na zingine.

Hatua hiyo imekuja baada ya Malawi kuzuia rasmi mazao ya kilimo kutoka Tanzania na Afrika Kusini kukataa kufungua soko lake la ndizi kwa zaidi ya miaka mitano, licha ya juhudi mbalimbali za kidiplomasia.

Miongoni mwa hatua nyingine zilizotajwa ni kusitisha usafirishaji wa mbolea kwenda Malawi, na kuzuia bidhaa za kilimo kutoka nchi hizo kupita Tanzania kuelekea bandari ya Dar es Salaam au maeneo mengine.

Waziri Bashe amesema hatua hizi ni za kulinda maslahi ya wakulima, wafanyabiashara wa Tanzania, na kuhakikisha usawa katika biashara za kikanda.

error: Content is protected !!