Migogoro zaidi ya 20,000 yapokelewa Kampeni ya Samia

HomeKitaifa

Migogoro zaidi ya 20,000 yapokelewa Kampeni ya Samia

Wizara ya Katiba na Sheria imesema migogoro 24,691 iliyodumu kwa muda mrefu ilipokelewa kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC), ambayo ilidumu kwa zaidi ya miaka 10.

Imesema utatuzi wa migogoro hiyo umewezesha kuimarisha amani, utulivu na utengamano miongoni mwa wanajamii kwa kuwa inaacha pande zilizokuwa na migogoro kuelewana.

Akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2025.2026 bungeni jijini Dodoma jana, Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Damas Ndumbaro alisema migogoro hiyo ilihusisha masuala ya ardhi, ndoa za utotoni, matunzo ya watoto, madai, ndoa, jinai, ukatili wa kijinsia, ardhi, ajira na mengineyo.

Aidha, alisema wameanzisha madawati ya msaada wa kisheria katika mamlaka za serikali za itaa 184, ambayo yamesaidia kusogeza huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi pamoja na uendelevu wa huduma ya msaada wa kisheria.

error: Content is protected !!