Tanzania kuzisaidia nchi tisa masuala ya utabiri hali ya hewa

HomeKitaifa

Tanzania kuzisaidia nchi tisa masuala ya utabiri hali ya hewa

Kutokana na Mamlaka ya Hewa Tanzania (TMA) kuendelea kuhimili viwango vya utoaji huduma kimataifa, Tanzania kupitia TMA imepewa jukumu la kusaidia nchi nyingine katika baadhi ya masuala ya uboreshaji wa huduma za hali ya hewa ikiwemo kuweka na kuendesha mifumo ya udhibiti ubora katika utoaji huduma maeneo ya usafiri wa anga, mifumo ya uchakataji, ubadilishaji na usambazaji data.

Nchi zilizosaidiwa hadi sasa ni Namibia na Burundi. Aidha, TMA imepokea maombi ya kuzisaidia nchi za Uganda, Zimbabwe, Sudan Kusini, Siera Leon, Gambia, Zambia na Guinea.

Katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2020 Ibara ya 59(j), serikali iliahidi kuendelea kuimarisha miundombinu na huduma za hali ya hewa ikiwemo ununuzi wa rada na vifaa vya hali ya hewa.

error: Content is protected !!