Tozo ya mafuta ilivyokamilisha ujenzi wa Daraja la Mawe la Mto Mmbaga

HomeKitaifa

Tozo ya mafuta ilivyokamilisha ujenzi wa Daraja la Mawe la Mto Mmbaga

Ujenzi wa daraja la mawe eneo la Mto Mmbaga unaounganisha kijiji cha Jema na kata ya Oldonyosambu wilayani Ngorongoro umesaidia kuondoa changamoto kwa wananchi katika usafirishaji wa mazao na huduma nyingine muhimu za kijamii.

Kwa mujibu wa wananchi wa eneo hilo akiwemo Abraham Maroseck na Abraham Mariseki walishukuru serikali kwa kutoa sh, milioni 500 kwaajili ya kutatua changamoto ya ukosefu wa daraja haswa nyakati za mvua na kupelekea mawasiliano awali kukatika haswa nyakati za mvua huku baadhi ya bidhaa kupanda bei kutokana na ukosefu wa daraja.

Daraja hilo lililogharimu shilingi milioni 500 ambazo ni tozo za mafuta limewezesha mazao haswa maharage, mahindi na huduma nyingine muhimu kufikika kwa haraka.

Aidha, daraja jilo limerahisisha usafiri kwa wananchi kutoka makao makuu ya mkoa, wilaya na kata za Sale, Pinyinyi na Oldonyosambu kupita Masusu, Oldonyosambu mpaka Jema ikiwemo kurahisiha mawasiliano katika kijijicha Jema na Kata ya Digodigo na Kirangi kupitia Oldonyosambu kuelekea Mkoa ni Arusha na Ngorongoro.

error: Content is protected !!