Zaidi ya wakazi 7,000 wa vijiji sita vya Gararagua na Kideco Kata ya Donyomorwa, wilayani Siha mkoani Kilimanjaro, wamepata ahueni baada ya serikali kulipatia ufumbuzi tatizo la kudumu la ukosefu maji safi na salama. Wakazi hao, walikuwa wakilazimika kutembea zaidi ya kilomita saba kila siku kufuata huduma hiyo vijiji jirani, hivyo kuathiri shughuli zao z akiuchumi na kijamii, hususan wanawake na wattoto.
Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Siha, Elikana Malisa, alisema wakazi wameondokana na adha hiyo baada ya kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa maji katika maeneo yao. Malisa, alisema mradi huo ni miongoni mwa miradi ya kimkakati inayotekelezwa kupitia fedha za Mfuko wa Maji wa Taifa (NWF).
Alisema mradi huo pia unatokana na fedha za Lipa Kulingana na Matokeo (P4R) na kutoa ajira za muda kwa watu 158, wakiwamo wanaume 152 na wanawake sita kutoka vijiji vya Sanya Juu, Merali, Ngumbaru, Naibili, Ngaritati na Loiwang.
Mradi huo wa majisafi na salama umegharimu shilingi bilioni 2.3.