Daraja la Masagi mkombozi kwa wananchi wa Iramba

HomeKitaifa

Daraja la Masagi mkombozi kwa wananchi wa Iramba

Kukamilika kwa daraja la Masagi linalojengwa katika barabara ya Kibirigi–Masagi kunatarajiwa kuunganisha vijiji vya Kibirigi, Masagi na Tyeme katika Kata ya Mtoa, Wilaya ya Iramba, mkoani Singida, na kufungua njia za mawasiliano na masoko ya mazao.

Meneja wa TARURA Mkoa wa Singida, Mhandisi Ibrahim Kibasa, amesema daraja hilo litasaidia wakulima na wafugaji wa eneo hilo kufikia masoko kwa urahisi, baada ya muda mrefu kukwama kutokana na kukosekana kwa kivuko cha uhakika katika Mto Sekenke.

“Vijiji hivi vinajishughulisha na kilimo cha pamba, alizeti, dengu na mahindi pamoja na ufugaji. Kukosekana kwa daraja kumekuwa kikwazo kwao katika kusafirisha mazao yao na kujiendeleza kiuchumi,” alisema Kibasa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi ya TARURA, CPA Ally Rashid, aliwataka wasimamizi wa mradi kuhakikisha ubora wa kazi na kuyashughulikia mapungufu yaliyobainika wakati wa ukaguzi.

error: Content is protected !!