Fursa za kibiashara Magomeni Kota

HomeKitaifa

Fursa za kibiashara Magomeni Kota

Rais Samia Suluhu Hassan amezindua nyumba 644 za Magomeni Kota leo Machi 23, 2022 na kuainisha fursa kadha wa kadha za kibiashara katika makazi hayo.

Magomeni Kota ndiyo makazi yenye watu wengi zaidi Tanzania, yakifuatiwa na yale ya Michenzani, Zanzibar na hivyo Rais awataka TBA kutumia hiyo kama fursa ya kibiashara.

Aidha, amewasifu Wakala wa Majengo Tanzania kwa mpango wa kujenga machinga complex na supermarket ndani ya makazi hayo na kuwataka kujenga maegesho yatayotumika kibiashara.

“Niwaombe mjenge ‘parking’ [maegesho] zile za kisasa, zitakazoweza kuweka magari mengi. Hii itakuwa ni kitega uchumi kwenu TBA. Anayetaka kulaza [gari] atalaza alipe, anayepaki kwa muda, atapaki alipe. Jengeni parking ya kisasa ili kukidhi haja ya ndani ya mji huu,” amesisitiza Rais Samia.

Ujenzi wa mradi wa Magomeni Kota umegharimu shilingi bilioni 52.2

error: Content is protected !!