Mgombea Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza kuwa Serikali yake itaanza ujenzi wa uwanja mkubwa wa ndege eneo la Kyabajwa, wilayani Misenyi, mkoa wa Kagera, katika kipindi cha miaka mitano ijayo akipewa ridhaa ya kuendelea kuongoza nchi.
Amesema uwanja huo utakuwa na uwezo wa kuhudumia ndege kubwa za abiria zenye uwezo wa kubeba watu 180 hadi 220, na utachochea maendeleo ya sekta za biashara, kilimo na utalii.
Dkt. Samia ameeleza kuwa awali eneo la Omukajunguti lilipendekezwa kwa ujenzi huo, lakini halikufaulu upembuzi yakinifu, hivyo ujenzi utafanyika Kyakabajwa.
Amesisitiza kuwa mradi huo ni sehemu ya mkakati wa serikali kuboresha miundombinu ya usafiri na kuimarisha sera ya kilimo biashara ili kuongeza fursa za uwekezaji na usafirishaji wa mazao nje na ndani ya nchi.