Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, ameishukuru Tanzania kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo na utulivu wa Uganda, akimtaja Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kuwa msingi muhimu wa mafanikio yanayoonekana nchini humo leo.
Akizungumza katika hotuba yake leo Mei 12, 2026 mara baada ya kuapishwa rasmi kuwa Rais wa Taifa la Uganda, Rais Yoweri Kaguta Museveni amesema wakati Uganda ikijivunia maendeleo yake ya sasa pamoja na uimara wa Jeshi la UPDF, ni muhimu kutambua mchango wa Tanzania na uongozi wa Mwalimu Nyerere katika kuweka msingi huo.
Aidha Rais Museveni alisema: “Msiisahau Tanzania,” akisisitiza umuhimu wa kuendelea kuthamini uhusiano wa kihistoria na ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili.


