Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Samia Suluhu Hassan amewataka maafisa wa Jeshi la Polisi kuhakikisha wanajenga taswira njema ya jeshi hilo kwa kuepuka vitendo vya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.
Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Mei 28, 2026 wakati akihitimisha mafunzo ya maafisa na wakaguzi wasaidizi wa Jeshi la Polisi katika Chuo cha Taaluma ya Jeshi la Polisi kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam.
Aidha, Rais Samia amewasisitiza wahitimu wa mafunzo, ambao ni maafisa na wakaguzi wasaidizi wa Jeshi la Polisi, kuwa mafunzo hayo yamewapa dhamana ya uongozi na watapimwa kwa nidhamu, weledi na matokeo katika kulinda raia na mali zao, si kwa vyeo walivyopewa.


