Serikali ya Tanzania yakanusha kuuza dhahabu

HomeKitaifa

Serikali ya Tanzania yakanusha kuuza dhahabu

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali haijawahi kuuza dhahabu iliyohifadhiwa katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), akieleza kuwa lengo la uhifadhi huo ni kuimarisha uchumi wa nchi na si kufanya biashara.

Akijibu swali Bungeni jijini Dodoma katika Kipindi cha Maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu amesema kwa sasa Tanzania ina hifadhi ya tani 27 za dhahabu ambazo zinaendelea kuwa sehemu ya akiba ya taifa.

Amesisitiza kuwa dhahabu hiyo haitauzwa kwa ajili ya kugharamia shughuli mbalimbali za Serikali, bali imehifadhiwa kama sehemu ya mizania ya uchumi na kuimarisha uwezo wa kifedha wa nchi.

error: Content is protected !!