Kulingana na matokeo ya sensa ya wanyamapori iliyotolewa na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI), Juni 17, 2026, Tanzania inaongoza bara la Afrika kwa kuwa ina idadi kubwa ya Simba.
Utafiti huo unaiweka Tanzania katika nafasi ya kwanza barani humo, ikiwa na jumla ya simba 17,200, ikifuatiwa na Afrika Kusini yenye simba 3,284 huku Kenya ikishika nafasi ya nne, ikiwa na jumla ya Simba 2,515.
Kwa upande mwingine, Tanzania imeendelea kuimarisha hadhi yake katika uhifadhi wa wanyamapori barani Afrika, kwa kuwa na Nyati wanaokadiriwa kufikia 328,000.


