Katambi: Iwe CCM au chama chochote, mikutano isitishwe

HomeKitaifa

Katambi: Iwe CCM au chama chochote, mikutano isitishwe

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Patrobas Katambi amemuelekeza Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Camillius Wambura kusitisha kwa muda vibali vya mikutano ya siasa hadi hapo itakapo tangazwa vingine.

Katambi ameyasema haya leo Juni 26,2026 Bungeni jijini Dodoma akieleza kuwa uchochezi wa kuhamasisha vurugu kabla na baada ya Sikukuu ya sabasaba umeonekana zaidi kuchochewa na masuala ya siasa hivyo mikutano yoyote ya hadhara isitishwe.

” Iwe chama Cha Mapinduzi, au chama chochote kile mikutano isitishwe, tutumie muda huu kuwaacha wananchi kufanya shughuli zao za kuwaingizia kipato” Amesema Katambi.

Amesema tayari jeshi la Polisi limekwisha wakamata baadhi ya wahalifu wanaohusika kwa namna moja ama nyingine kuhamasisha vurugu, hivyo amemuelekeza IGP Wambura kufuatilia Maeneo yote yanayotiliwa mashaka ikibidi kuyafungia shughuli zao kwa muda hadi yatakapochunguzwa.

error: Content is protected !!