Waokota 3,000 taka kusajiliwa

HomeKitaifa

Waokota 3,000 taka kusajiliwa

Wakati waokota taka 3,000 katika mikoa 12 ya Tanzania Bara wakitarajiwa kusajiliwa katika programu ya kidigitali ya Zaidi, unyanyapaa umetajwa kuwa changamoto kubwa kwao.

Kusajiliwa kwao ni hatua ya awali ya utambuzi wa watu hao ambao wanategemewa katika urejelezaji taka kwani asilimia 60 ya malighafi ya viwanda vya urejelezaji inatoka kwao.

Hilo linafanyika ikiwa ni maadhimisho ya siku ya waokota taka duniani iliyofanyikwa katika wiki iliyopita.

“Ingawa mchango wao ni muhimu, watu hawa wanakabiliwa na changamoto nyingi na vitisho katika maisha yao. Hawa ni miongoni mwa makundi yaliyo hatarini yanayokabiliwa na unyanyapaa na ukosefu wa usaidi nchini,” alisema Allen Kimambo, mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Taka ni Ajira.

Albert Kalugendo, mwokota taka wa Pugu jijini hapa aliomba waokota taka kupewa vifaa kinga ili viwasaidie kujikinga maradhi.

error: Content is protected !!