Frank Sempombe, mwanafunzi wa Kidato cha Tano katika Shule ya Sekondari Mkongo Wilaya ya Rufiji, amefariki dunia kwa kujinyonga karibu na eneo la shule.
Polisi wamesema mwili wa mwanafunzi huyo ulikutwa unaning’inia juu ya mti na hakuacha ujumbe wowote.
“Jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi kuhusiana na tukio hilo. Mwili wa marehemu umefanyiwq uchunguzi na daktari ili kuthibitisha chanzo cha kifo chake,” imesema taarifa ya Polisi.
Aidha, Polisi wametoa rai kwa wazazi na walezi kuwa karibu na watoto wao kujua changamoto zinazowakabili k kuepuka watoto wao kuchukua maamuzi magumu ya kusitisha uhai wa maisha yao.


