Mwanafunzi auawa, akatwa kiganja Pemba

HomeKitaifa

Mwanafunzi auawa, akatwa kiganja Pemba

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba limesema linaendelea na uchunguzi wa tukio la kuuawa kwa mwanafunzi wa kidato cha kwanza, Raiyan Hemed Amour, mwenye umri wa miaka 15, mkazi wa Kijiji cha Kwale Mpona, Shehia ya Finya, Wilaya ya Wete.

Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi iliyotolewa Oktoba 5, 2026, mwili wa mwanafunzi huyo ulikutwa kichakani ukiwa na jeraha kwenye kiganja cha mkono wa kulia, linalodaiwa kusababishwa na kitu chenye ncha kali.

Polisi wamesema Oktoba 2, 2026, Raiyan aliondoka nyumbani kuelekea shuleni lakini hakurejea. Baadaye baba yake aliripoti kupotea kwake katika Kituo cha Polisi Wete na uchunguzi ukaanza.

Mwili wake ulipatikana baadaye na kufanyiwa uchunguzi katika Hospitali ya Wilaya ya Wete, Kinyasini, kabla ya kukabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi.

Polisi wamesema wanaendelea kuwatafuta na kuwakamata wanaodaiwa kuhusika na tukio hilo.

error: Content is protected !!