Mahakama yahukumu watatu kwenda jela miaka 30 kwa unyang’anyi wa kutumia silaha

HomeKitaifa

Mahakama yahukumu watatu kwenda jela miaka 30 kwa unyang’anyi wa kutumia silaha

Mahakama ya Wilaya ya Kyela, Mbeya imewahukumu kifungo cha miaka 30 jela Boniface Charles, mkazi wa Ibanda, Sadick Mwanyemba, mkazi wa Itope na Biko Mwabulambo mkazi wa Kajunjumele kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha.

Washitakiwa walitenda kosa hilo Januari 01, 2026 saa 7 usiku, baada ya kumvamia mzee mwenye umri wa miaka 80 nyumbani kwake na kumshambulia kwa panga, rungu na nondo kisha kumpora baadhi ya mali zake.

Mali hizo ni pamoja na simu mbili, begi la nguo, tochi, kadi nne za banki pamoja na pesa taslimu walizotoa kwenye akaunti za mlalamikaji, na baada ya kutekeleza uhalifu huo walitokomea kusikojulikana.

Mwendesha mashitaka wa Serikali, wakili Brice Kessy akiwa mahakamani hapo aliiomba Mahakama kutoa adhabu kali kwa mujibu wa sheria ili iwe fundisho kwa watuhumiwa na watu wengine wenye tabia kama za watuhumiwa.

error: Content is protected !!