Mahakama yatengua amri ya kumkamata na kumrudisha Tanzania Sativa

HomeKitaifa

Mahakama yatengua amri ya kumkamata na kumrudisha Tanzania Sativa

Mahakama Kuu ya Tanzania imetengua amri ya kukamatwa na kurejeshwa nchini kwa mwanaharakati wa mitandaoni, Edger Mwakabela maarufu kama Sativa, ikisema amri hizo hazikuwa halali kisheria.

Uamuzi huo umetolewa Septemba 29, 2026 na Jaji wa Mahakama Kuu, Dafina Ndumbaro, baada ya kusikiliza rufaa ya Sativa dhidi ya uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Jaji Ndumbaro amesema hati ya kukamatwa pamoja na maagizo ya kumrejesha Sativa kutoka Kenya kwenda Tanzania hayakuwa na nguvu za kisheria na hayawezi kutekelezwa.

Kwa mujibu wa hukumu hiyo, mahakama imebaini kuwa mwenendo wa shauri katika mahakama ya chini ulikiuka taratibu za kisheria, ikiwemo kuendesha kesi bila mamlaka sahihi na kwa kutumia hati yenye kasoro za kisheria.

Sativa, kupitia wakili wake Jebra Kambole, alipinga uamuzi wa Mahakama ya Kisutu, akidai kuwa shauri liliendeshwa bila yeye kuitwa au kupewa nafasi ya kusikilizwa.

Pia, amedai kuwa hakuwahi kupewa wito wa mahakama wala kufikishiwa taarifa kwa utaratibu unaotakiwa kisheria.

 

error: Content is protected !!