Jamhuri yasema uchunguzi kesi ya Rugemalira haujakamilika

HomeKitaifa

Jamhuri yasema uchunguzi kesi ya Rugemalira haujakamilika

Kesi  ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa VIP na mmiliki mwenza wa zamani wa kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), James Rugemalira na mwenzake (Joseph Makandege) imeahirishwa hadi 23, 2021.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya wakili wa Serikali Faraja Ngukah kuieleza mahakama kwamba upelelezi bado haujakamilika.

Hayo yamejiri leo  Septemba 9, 2021 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa  mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Hata hivyo washtakiwa hao (Rugemalira na Makandege ambaye alikuwa mwanasheria wa IPTL) hawakufikishwa Mahakamani hapo kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo.

error: Content is protected !!