Kocha wa Chelsea, Thomas Tuchel aeleza anapokosea Arteta

HomeMichezo

Kocha wa Chelsea, Thomas Tuchel aeleza anapokosea Arteta

‘Kila uwezo unapoongezeka, ndio majukumu huwa makubwa zaidi,’ ndicho hasa kinachomsibu Arteta Arsenal. Ikumbumkwe kuwa Arteta ametoka kuwa mwalimu msaidizi kutoka klabu ya Manchester City na moja kwa moja kuwa mwalimu mkuu kunako washika bunduki wa London, Arsenal.

Arteta alipendekezwa kwa kazi ya kukinoa kikosi cha Arsenal ambacho sasa kinashika mkia kwenye Ligi Kuu ya England, Septemba 2020, lengo likiwa ni kufanya kazi na Edu, na so chini yake.

CEO wa Arsenal, Vinal Vankatesham aliamini kwamba Edu kufanya kazi pamoja na Arteta kutazaa matunda, lakini kutokuwa na uzoefu wa kutosha kwa Arteta kwenye kazi ya ukocha ni tatizo kubwa sana kwa Arsenal hivi sasa, wapo waliotema nyongo tangu siku Arteta anatangazwa kuwa hafai.

Wakati ambapo bado hana uzoefu na kazi hiyo, bada anamajukumu mengine kama kusajili, kuuza wachezaji, kuangalia afya zao na mambo mengine mengi ambayo yanamfanya asiwe makini kwenye kazi yake. Hivyo, ingetakiwa afanye kazi chini ya Edu na sio kufanya naye kazi.

Hii ni tofauti kwa Chelsea ambapo Thomas Tuchel anafanya kazi chini ya Mkurugenzi wa Ufundi, Marina Granovskaia. Marina yeye anahusika na kusajili na kazi yake imeonekana akisajili mtu kama Kai Havertz, Thiago Silva, Timo Werner, Ben Chilwell na Romelu Lukaku. Tuchel kazi yeye ni kufundisha tu, tofauti na Arteta mwenye mzigo mkubwa wa kazi Arsenal.

Tuchel amekaririwa akisema anafuraha sana Chelsea, na mfumo huo umechangia sana Chelsea kushinda kikombe cha Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) licha ya kwamba Tuchel alianza kazi Chelsea katikati ya msimu.

“Kazi yangu imekuwa rahisi sana Chelsea, hapa nafundisha tu. Sina jukumu la kuhakikisha ni nani anakuja au nani anaondoka”.. ameongeza Tuchel.

error: Content is protected !!