Tetesi za soka Ulaya leo Septemba 23 (Rudiger kwenda Munich, Asensio kutua Liverpool)

HomeMichezo

Tetesi za soka Ulaya leo Septemba 23 (Rudiger kwenda Munich, Asensio kutua Liverpool)

Bayern Munich wana nia ya kumsajili beki wa Chelsea na Ujerumani Antonio Rudiger, lakini mchezaji huyo wa miaka 28 anataka kusaini mkataba mpya huko Stamford Bridge (Bild – German).

Barcelona italazimika kulipa euro milioni 1.8 (£ 1.5m) ili kumtoa Roberto Martinez kutoka kwa mkataba wake na timu ya taifa ya Ubelgiji. (Sport – Spanish).

FC Basel inafikiria kumchukua mlinda lango wa Liverpool na Ujerumani Loris Karius, 28 (Bild – German).

Manchester City wamekataa dau la pauni milioni 15 kutoka Borussia Dortmund kwa mshambuliaji wa England Liam Delap, 18 (Football Insider).

Klabu ya Arsenal na AC Milan wanawania saini ya winga wa Uholanzi anayechezea Club Brugge ya Ubelgiji Noa Lang, 22 (Express).

Martinez amepuuza ripoti zinazomuhusisha na kazi ya kuinoa Klabu ya Barcelona kama mbadala anayeweza kuchukua nafasi ya Mholanzi aliye chini ya shinikizo Ronald Koeman, 58 (Eurosport).

Liverpool wanamtazama winga wa Real Madrid na Uhispania Marco Asensio, 25 (Fichajes – Spanish).

Kocha wa Chelsea Thomas Tuchel amedokeza kwamba kiungo wa England Ruben Loftus-Cheek, 25, anapaswa kumvutia ili kutetea nafasi yake ndani ya kikosi hicho (Express).

error: Content is protected !!