Leo katika historia: Daktari bingwa wa magonjwa ya akili anafariki dunia

HomeElimu

Leo katika historia: Daktari bingwa wa magonjwa ya akili anafariki dunia

Tarehe kama ya leo mwaka 1908: Chuo Kikuu cha Alberta kilianzishwa nchini Canada. Chuo hicho kilianzishwa na Alexander Rutherford na Henry Marshall Tory.

Mwaka 1939, Sigmund Freud aliaga dunia, alikuwa daktari wa magonjwa ya akili, raia wa Austria. Sigmund alizaliwa mwaka 1856. Daktari huyo alifanya utafiti na kuchunguza matatizo mbalimbali ya kiakili yanayowakumba binadamu na kutoa maoni na nadharia mpya kuhusu chanzo cha magonjwa ya akili. Kwa sababu hiyo anahesabiwa kuwa mwasisi wa elimu ya uchunguzi wa kisaikolojia au Psychoanalysis.

Mwaka 1920: Alexander Millerand alichaguliwa kuwa Rais wa Ufaransa. Kiongozi huyo alitawala kwa miaka minne tu. Awali, Millerand alikuwa Waziri Mkuu wa Ufaransa kati ya Januari na Septemba, mwaka huo.

Miaka 346 iliyopita katika tarehe kama ya leo, Valentin Conrart, mwandishi na mwanafasihi wa Kifaransa aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 72. Alizaliwa mwaka 1603 katika familia iliyokuwa na mapenzi makubwa na fasihi ya lugha na kwa msingi huo ndio maana alipokuwa katika rika la ujana, Valentin Conrart akawa na mapenzi na taaluma ya fasihi ya lugha na taratibu akaanza kujihusisha na fani ya uandishi.

error: Content is protected !!