Rais Samia ahimiza kuimarishwa biashara kati ya Tanzania na Marekani

HomeKitaifa

Rais Samia ahimiza kuimarishwa biashara kati ya Tanzania na Marekani

Rais Samia Suluhu Hassan amewahimiza na kuwaeleza wafanyabiashara wa Tanzania na Marekani kuimarishwa ushirikiano wa kibiashara kati ya mataifa hayo mawili ili kuwa na faida kwa pande zote.

Amesema hayo aliposhiriki mkutano wa pamoja kati ya wafanyabiashara wa Tanzania na Marekani Septemba 22, 2021 na kusisitiza kwa sasa biashara zinazofanyika kati ya Tanzania na
Marekani ni ndogo ikilinganishwa na fursa zilizopo.

Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2019, Tanzania iliagiza bidhaa zenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 241 (TZS 558 Bilioni) na kuuza bidhaa zenye thamani ya dola za kimarekani milioni 46 (TZS 106 Bilioni). Kwa upande mwingine Marekani imewekeza Tanzania Dola za Kimarekani bilioni 5.55 (TZS 12 Trilioni) na kuajiri watu 44,118 wakati Tanzania imewekeza kiasi cha Dola za Kimarekani milioni moja tu ambacho ni kiasi kidogo ikilinganishwa na ukubwa wa uchumi wa Marekani duniani na fursa zilizopo Tanzania.

Rais Samia amewaeleza wafanyabishara hao kuwa angependa kuona biashara inaongezeka kwa kuwa Tanzania ni mwanachama katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na pia Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ambazo zinatoa fursa za wawekezaji na wafanyabishara wa Marekani kwa soko la watu milioni 450, hivyo kuwa na mazingira mazuri ya uwekezaji.

error: Content is protected !!