Vanessa Mdee ashambuliwa kisa wigi alilovaa.

HomeBurudani

Vanessa Mdee ashambuliwa kisa wigi alilovaa.

Katika sehemu ambayo kuna wajuaji wa kila kitu basi ni Instagram hasa kama wafuasi wako ni kutoka hapa Tanzania. Hili linathibitishwa na kilichomtokea mwanadada Vanessa Mdee  Tanzania baada ya kuweka picha kwenye ukurasa wake wa Instagram siku ya jana akiwa na mpenzi wake mwigizaji kutokea Marekani, Rotimi.

Baada ya Vannesa “ku-post” picha hiyo “followers” wake wengi walivamia sehemu ya “ku-comment”  na kuanza kumtolea povu na kumchamba kuhusu wigi ambalo ameonekana nalo, wakidai kuwa inabidi atafute mtaalamu wa nywele ili awe anamsaidia kwenye muonekano wake.

error: Content is protected !!