Mbwa mwitu waiba begi la Shakira

HomeBurudani

Mbwa mwitu waiba begi la Shakira

Mwanamuziki kutoka nchini Colombia, Shakira ambaye pia ni mke wa Gerald Pique, mchezaji wa FC Barcelona, ameleza jinsi alivyovamiwa na mbwa mwitu akiwa na mtoto wake, Millan katika hifadhi ya wanyama Barcelona.

Mshindi huyo wa tuzo 333 za muziki amesema kwamba mbwa mwitu hao walimvamia na kuondoka na begi lake lililokuwa na vitu vyake ikiwemo simu, hata hivyo ameweza kulipata likiwa limeharibika sana.

Kutokana na tukio hilo Polisi jijini Barcelona wamesema kuwa kweli kuna malalamiko kuhusu wanyama hao kwani sio mara ya kwanza mtu kuvamiwa na mbwa mwitu huku wakieleza chanzo ni ongezeko la wanyama hao.

error: Content is protected !!