Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 03 (Cavani mbioni kujiunga Real Madrid, Fekir kutua Arsenal)

HomeMichezo

Tetesi za Soka Ulaya leo Oktoba 03 (Cavani mbioni kujiunga Real Madrid, Fekir kutua Arsenal)

Paris St-Germain wameripotiwa kujitoa katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Norway, Erling Haaland (21) kutoka Borussia Dortmund msimu ujao (Mirror).

Kiungo wa kati wa Leeds Kalvin Phillips (25) yupo tayari kutia saini mkataba mpya ulioboreshwa kuitumikia klabu hiyo. Mchezaji huyo bado ana mkataba wa miaka 2 kwa sasa (Athletic).

Mshambuliaji wa Manchester United Edinson Cavani 34, anaweza kujiunga na Real Madrid dirisha dogo la usajili Januari, baada ya kutopata nafasi ya kucheza Old Trafford kufuatia kuwasili kwa Cristiano Ronaldo (Mundo Deportivo – Spanish).
>Tetesi za soka Ulaya leo Oktoba 02 (Henry akosoa kauli ya Wenger, Sterling njia panda Man City)

Steve Bruce atabaki kuwa meneja wa Newcastle kwani kipaumbele cha mmiliki wake, Mike Ashley inabaki kupata mnunuzi wa klabu hiyo (Sun).

Manchester City wanaamini wana nafasi kubwa dhidi ya wapinzani wao Liverpool, Manchester United, Chelsea na Bayern Munich katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Benfica Darwin Nunez, 22 (Star).

Manchester United wanahitaji wawe wamefikia maamuzi ya mwisho juu ya mustakabali wa kiungo wa Ufaransa Paul Pogba kabla ya sikukuu ya Christmas (Sun).

Barcelona inaangalia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Manchester City Raheem Sterling 26, dirisha dogo la usajili januari (OnzeTV kwenye Twitter).

Real Madrid inafikiria kufanya usajili wa kiungo wa Leicester, Youri Tielemans 24, lakini kuwasili kwake kunatoa nafasi ya kuondoka kwa kiungo wa Brazil Casemiro 29, kwenda Paris St-Germain (El Nacional).

Kiungo wa Cagliari Nahitan Nandez (25) anatarajiwa kuondoka, kulingana na wakala wake. Mchezaji huyo amepokea ofa kutoka klabu Tottenham, Leeds na Napoli (Calcio Napoli – 24).

Mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema (33) amesema anaamini, mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe, 22, atajiunga naye Real Madrid siku moja (L’Equipe – Sun).

West Ham, Everton na Arsenal wapo katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Real Betis Nabil Fekir (28) lakini Betis bado wana nia ya kupata huduma za Mfaransa huyo (Fichajes – Spanish).

Bayern Munich wanakaribia kukubali mkataba mpya na mshambuliaji wake Serge Gnabry, 26 (Fabrizio Romano, Twitter).

error: Content is protected !!