Hizi ni nyimbo 5 ambazo hazipitwi na wakati nchini

HomeBurudani

Hizi ni nyimbo 5 ambazo hazipitwi na wakati nchini

Katika tasnia ya muziki hivi sasa wadau wengi wamekuwa wakitoa maoni yao kuhusu nyimbo zinazotungwa na wasanii wa kizazi kipya kuwa hazikai muda mrefu, zinasikilizwa na kupotea kwa muda mfupi.

Zifuatazo ni nyimbo ambazo zilitungwa miaka mingi na bado zinaendelea kupendwa na kusikilizwa mpaka sasa.

1. Mkono wa Idd Salum Abdallah
Wimbo huu una zaidi ya miaka 60 tangu kutungwa kwake ila mpaka sasa unatumika kwenye sherehe za sikukuu ya Idd kutokana na tungo zake. Mwimbaji wake Idd Salum alifariki mwaka 1965 katika ajali ya gari Morogoro.

2. Christmas wa King Kiki
Unapofika msimu wa sikukuu za Christmas wimbo huu lazima upigwe, lakini ulitungwa tangu katikati ya miaka ya 70 na msanii King Kiki akiwa na bendi yake ya Maquiz Du Zaire.

3. Siku ya kufa Dkt. Remmy Ongalla 
Remmy Ongalla ni maarufu hata katika kizazi hiki ambacho akikumshuhudia kutokana na kuwa na nyimbo nyingi ambazo bado zinaendelea kufanya vizuri mpaka sasa hivi. Siku ya Kufa ulitungwa miaka ya 70 akiwa na Orchestra Makassy.

         > Video 5 za Tanzania zinazo-trend YouTube leo Oktoba 03, 2021

5. Noeli King Kiki
Miaka ya 80 King Kiki alihamia Orchesta Safari Sound na kutunga wimbo mwingine ambao unaongelea sikukuu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo unaoitwa Noeli.

5. Kifo Dk Remmy Ongalla
Pamoja na kwanza akishakuwa na wimbo unaoelezea kifo, miaka ya 80 alitoa tena wimbo unaolezea kifo alioupa jina la kifo. Wimbo ni maarufu zaidi na unapigwa sana vinavotokea vifo vya viongozi wakubwa au wasanii. Remmy Ongalla alifariki mwaka 2010.

error: Content is protected !!