Video 10 za wanamuziki wa Tanzania zilizotazamwa zaidi YouTube mwaka huu

HomeBurudani

Video 10 za wanamuziki wa Tanzania zilizotazamwa zaidi YouTube mwaka huu

Ikiwa imetimia robo tatu ya mwaka 2021 kuelekea ukingoni mwa mwaka huu, wasanii wa BongoFleva kutoka nchini Tanzania wameonesha kukimbiza kwa video za baadhi ya nyimbo zao kwenye mtandao wa Youtube. Hizi ni video za nyimbo 10 zilizotazwa zaidi tangu Januari mwaka huu kwenye mtandao YouTube.

1. Sukari- Zuchu
Video ya wimbo huu iliachiwa Januari 30, 2021 ikiongozwa na Kenny, tayari imejikusanyia watazamaji milioni 53 huku ikivunja rekodi ya kuwa wimbo wa msanii wa kike uliotazamwa zaidi.

2. Baikoko- Mbosso
Ni wimbo huu unapatikana  kwenye albamu yake “Definition of Love”, video yake ilitoka April 9, 2021. Mpaka sasa ina watazamaji milioni 24.7.

3. Attitude- Harmonize
April 23, 2021 ndipo ilitoka video ya wimbo huu aliyoshirikiana na  Awilo Longomba na H.Baba. Ni video namba 3 ina watazamaji milioni 13.4.

4. Nyumba Ndogo- Zuchu
Ikiongozwa na Hanscana mpaka sasa video hiyo ina watazamaji milioni 11.9 tangu iachiwe Julai 1,2021.

5.Yalah- Mbosso
Ikiwa na watazamaji milioni 10.9 tangu iachiwe Machi 13,2021. Huu ni kati ya nyimbo zinazopatikana kwenye albamu yake ‘Definition of Love’.

> Hizi ni nyimbo 5 ambazo hazipitwi na wakati nchini

6. Iyo- Diamond Platnumz
Ni wimbo aliyoshirikishwa Focalistic, Mpara A Jazz na Ntosh Gazi chini ya mtayarishaji Hanscana. Tangu kuachiwa kwa video yake Julai 29, 2021 imetazamwa na watu milioni 9.8.

7. Kiuno- Rayvanny
Kutoka kwenye albamu yake ya ‘Sound From Africa’ video ya wimbo huu ilitoka Februari 10, 2021. Ikiongozwa na mtayarishaji Kenny video yake imepata watazamaji milioni 8.4.

8. Jenifa- Rayvanny
Akifanya remix ya wimbo wa mwanadada Guchi kutoka nchini Nigeria na kumshirikisha, video hiyo imefanya vizuri na kupata watazamaji milioni 8..

9. Jealous- Ali Kiba
Mwongozaji Pink kutoka Lagos, Nigeria ndiye alikamilisha video ya wimbo huu aliyoshirikisha  msanii Mayorkun kutoka nchini humo ambayo imetazwa na mara milioni 7.98.

10. Sandakalawe- Harmonize
Zaidi ya watazamaji milioni 7.1 wameweza kutazama video ya msanii huyu kutoka Konde Gang Music label wenye mahadhi ya Amapiano.

Wanamuziki  Zuchu, Mbosso, Rayvanny na Harmonize wamekuwa na wakati mzuri zaidi kwenye mtandao wa Youtube, kwani wameweza kuingiza video mbili kwa kila mmoja kwenye orodha hii.

error: Content is protected !!