Afariki baada ya kulipukiwa na bomu aliloliokota

HomeKimataifa

Afariki baada ya kulipukiwa na bomu aliloliokota

Mtu mmoja mwenye asili ya Ujerumani amefariki dunia nchini Australia baada ya kulipukiwa na bomu ambalo aliliokota ziwani.

Mtu huyo mwenye umri wa miaka 59 aliokota kilipizi hicho pasi na kujua kuwa ni bomu na kukiweka pembezoni mwa ufukwe wa ziwa. Bomu hilo likiwa limechakaa kwa kutu, mzee huyo inasemekana kwamba alilichukua ili achunguze kutaka kujua ni kitu gani. Siku ya pili aliendeA kifaa kile kwa ajili ya kukichunguza, na hatimaye kililipuka na kuchukua uhai wake.

> Hamar, Kabila la Ethiopia lenye mila za kustaajabisha

Wenyeji waishio pembezoni mwa ziwa hilo, wamesema kuwa licha ziwa hilo kuwa maarufu sana kwa watu wanaopenda kuogelea, lakini ziwa hilo pia ni maarufu kutokana na kuwa na mabaki mengi ya mabomu yaliyotumika kwenye vita vya pili ya dunia kati ya Ujerumani na Uingereza.

Katika mwaka 2020 pekee, kitengo cha kutegua mabomu cha jeshi la Australia liliibua tani 28.7 za mabaki ya sihala zilizotumika vita ya pili ya dunia.

error: Content is protected !!