Mwanasheria mbaroni tuhuma za mauaji ya mpenzi wake

HomeKitaifa

Mwanasheria mbaroni tuhuma za mauaji ya mpenzi wake

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara linamshikilia Mwanasheria Keneth Nkiko (28) kwa tuhuma za kumuua Magreth Richard (22), mfanyabiashara na mkazi wa Mkendo, Manispaa ya Musoma Mjini, mkoani Mara.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Pius Lutumo amesema tukio hilo limetokea Oktoba 5, 2026, katika Mtaa wa Mwigobero, Manispaa ya Musoma Mjini.

Kamanda Lutumo amesema Nkiko ambaye jukumu lake lilikuwa kutoa msaada wa kisheria kwa waathirika wa vitendo ukatili wa kijinsia anadaiwa kumuua binti huyo ambaye alikuwa ni mpenzi wake kwa kumpiga na kitu butu kichwani kisha kumchoma na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake.

Ameongeza kuwa uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha tukio hilo ni wivu wa mapenzi, ambapo mtuhumiwa alikuwa akimtuhumu mpenzi wake kuwa anamsaliti kwa kuingiza wanaume wengine ndani wakati yeye hayupo.

 

error: Content is protected !!