Rais Samia afikisha Daraja la JPM 74%

HomeKitaifa

Rais Samia afikisha Daraja la JPM 74%

Miaka miwili ya Rais Samia Suluhu Hassan, daraja la JP Magufuli limefikia asilimia 74 ya ujenzi wake, ambapo mpaka sasa Sh bilioni 368.671 zimetolewa kwa Mkandarasi China Civil Engineering.

Mkurugenzi wa Miradi na Maendeleo Tanroads, Mhandisi Boniface Mkumbo, amesema wakati Rais Samia ameingia madarakani ujenzi wa daraja hilo ulikuwa asilimia 26 na kiasi ambacho kilitolewa ni Sh bilioni 118.

“Daraja hili litaanza kutumika rasmi Februari 24, 2024,” amesema Mkumbo katika kongamano la miaka miwili ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan linaloendelea mkoani Mwanza. Daraja hilo linaunganisha eneo la Kigongo wilayani Misungwi na Busisi wilayani Sengerema.

error: Content is protected !!