Raia 57 wa Kenya wanaswa katika operesheni ya Loliondo

HomeKitaifa

Raia 57 wa Kenya wanaswa katika operesheni ya Loliondo

Operesheni Maalum ya siku 10 iliyofanywa na Jeshi la Uhamiaji katika Tarafa za Sale na Loliondo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha, imewanasa watu 72 walioingia nchini kinyume na sheria.

Jeshi hilo pia limefanya ukaguzi wa shuguli mbalimbali za mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NGO) yaliyoko katika tarafa hizo mbili.

Kwa mujibu wa Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Arusha , Kamishina Msaidiziwa Uhamiaji (ACI), Hosea Kagimbo, waliokamatwa ni raia wa Kenya 57, raia wa Ufaransa saba na walowezi wanane.

Kagimbo alisema kati ya watuhumiwa hao, 30 watafikishwa mahakamani huku 13 wakiachiwa huru ilhali wengine 29 uchunguzi bado unaendelea.

Hata hivyo, Kagimbo alisema zoezi hilo limekabiliwa na vikwazo vya baadhi ya watu kuyakimbia maboma yao na uchunguzi unaendela kuwasaka.

Serikali imepunguza ukubwa wa Pori tengefu la Loliondo kutoka kilometa za mraba 4,000 hadi kilometa za mraba 1,500 huku ikiacha kwa wananchi kilometa za mraba 2,500.

 

error: Content is protected !!