Jeshi la Magereza limesema Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu yupo salama na hayuko kwenye mgomo wa kula chakula kama ilivyoripotiwa na baadhi ya viongozi wa chama hicho.
Aidha, limesema Lissu ameendelea kutembelewa na mawakili wake wanaomwakilisha na wameendelea wameruhusiwa kuonana na mteja wao baada ya kujiridhisha kuwa ni mawakili wake na si vinginevyo.
“Katika kutekeleza majukumu yake ya kuwapokea, kuwahifadhi na kuwarekebisha wale wote wanaoshikiliwa magerezani, wakati wote Jeshi limekuwa likizingatia mambo yote yanayohusu usalama wao kwa kipindi chote wanachokuwa chini ya ulinzi halali wa Jeshi la Magereza,” limesema.
Hata hivyo, Jeshi limetoa rai kwa wananchi kupuuzia taarifa hiyo na kuacha kusambaza taarifa isiyo na ukweli kwakuw ni kosa kisheria.


