NIDA kufuta matumizi ya namba, yatoa miezi mitatu

HomeKitaifa

NIDA kufuta matumizi ya namba, yatoa miezi mitatu

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imetoa miezi mitatu wananchi wanaotumia namba za NIDA kufuata vitambulisho kwani baada ya muda huo itafuta matumizi ya namba hizo.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa Kitambulisho cha Taifa kilichoboreshwa, Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, James Kaji amesema wananchi wengi hawajafuata vitambulisho vyao licha ya kutangaza kila mara kwenye vyombo vya habari.

Aidha, amewataka wananchi wenye vitambulisho vilivyofutika maandishi kufika katika vituo vya NIDA vilivyopo karibu nao ili kupewa vitambulisho bila malipo yoyote.

error: Content is protected !!