Wanaotumia mvuke kujisafisha uke hatarini

HomeKitaifa

Wanaotumia mvuke kujisafisha uke hatarini

Madaktari wameonya mataumizi ya njia za kujifukiza ukeni wakisema huua bakteria walinzi na kuweka hatarini kupata mambukizi ya magonjwa. Kauli ya wataalamu hao wa afya imekuja baada ya baadhi ya watu kutangaza biashara ya kujifukiza katika mitandao ya kijamii.

Akizungumza suala hilo, Dkt. Samweli Shita anasema kama njia ingekuwa sahihi na muhimu, basi ingekuwa ikitumika hata katika hospitali za wilaya na mikoa. “Sijawahi kuona andika ambalo linaonesha kuwa njia hii ni sahihi.” alisema Dkt Shita.

Alisema hizo inawezekana ni tiba mbadala ambazo watu wamezibuni kama njia za kujiongezea kipato. Daktari alitumia njia hizo kuwatahadharisha wanawake wanaotumia njia hizo kuwa kwa kufanya hivyo huua kinga ya uke. Alisema pia ukeni kuna tindakali ambayo haitakiwi kuvurugwa kwa kuingiza chochote, kwani kufanya hivyo na marekebisho ya bakteria na fangasi.

Dkt Isaya Mhando, ambaye ni daktari wa magonjwa ya wanawake kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MHF) anasema uke unajisafisha wenyewe, huku akishauri kuwa ni vyema watu wakaonana na daktari pindi wanapojihisi kuumwa. “Lakini kama mtu ana tatizo la kutokwa uchafu ukeni, ni vyema kuchukua sampuli ya uchafu ule na kuupeleka maabara kujua mtu huyo anasumbuliwa na bakteria wa aina gani, hapo tutaweka kumpatia tiba kulingana na tatizo linalomsibu nasi vingineyo”. Alimalizia daktati

error: Content is protected !!