Madini bado yanatoroshwa

HomeKitaifa

Madini bado yanatoroshwa

Licha ya Serikali kutangaza kuziba mianya ya utoroshaji wa madini, baadhi ya wabunge wamesema bado rasilimali hiyo inatoroshwa. Mjadala huo mzito umeibuliwa Bungeni jijini Dodoma wakati wa mjadala wa kuchangia mapendekezo ya mwongozo wa Mpango wa Maendeleo wa Serikali mwaka 2022/2023.

Waziri wa Madini Dkt. Dotto Biteko alisema utoroshwaji wa madini umedhibitiwa kwa kiasi kikubwa na hata wanaojifanya kutorosha hushindwa kupata soko.
Biteko pia ameongeza kusema kuwa ukuwaji wa sekta hiyo ya madini mwaka 2019 ni asilimia 17.7 na kuwa ya kwanza kwa ukuaji nchini, ikilinganishwa na kipindi cha nyuma kabla ya uhuru.

Mchango wa sekta hiyo kwenye pato la Taifa umeongezeka kutoka asilimia 3.8 mwaka 2014 hadi kufikia asilimia 5.2 mwaka 2019, alisema na kuongeza kabla ya mwaka 2000, wastani wa mchango wa sekta hiyo ilikuwa ni asilimia 3. Pia Waziri Biteko ameongeza kuwa mchango wa wachimbaji wadogo wa dhahabu kwenye makusanyo ya maduhuli ya Serikali umeongezeka kutoka asilmia 10 mwaka 2017/2018 hadi asilimia 27 mwaka 2020/2022.

error: Content is protected !!