Maambukizi ya Ukimwi yaongezeka

HomeKitaifa

Maambukizi ya Ukimwi yaongezeka

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi imewataka wahusika wote wa utoaji elimu na zana za kupambana na maambukizi na ueneaji wa kasi wa Ukimwi kufanya kazi kama inavyotakiwa bila kusubiri ripoti ya kamati.

Ripoti hiyo kuwa maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI kwa mikoa ya Mwanza na Geita yameongezeka hadi kufikia 7.2% na 6.4%  mtawalia ikilinganishwa na  4.7% ya maambukizi kitaifa.

Sababu kadha wa kadha zimetajwa kuwa chanzo cha maambukizi hayo katika ripoti iliyowasilishwa bungeni mapema leo ikiwemo kukosekana kw elimu ya kutosha kuhusu UKIMWI kwenye mialo.

Mengine yaliyotajwa ni pamoja na  ukosekana kwa kondomu katika sehemu za kulaza wageni (guest house) na uhaba wa msaada toshelezi kwa waathirika wa VVU.

Ukimwi upo. Jilinde, mlinde na mwingine.

error: Content is protected !!