Spika Ndugai ampa onyo kali Jenerali Ulimwengu

HomeKitaifa

Spika Ndugai ampa onyo kali Jenerali Ulimwengu

Mwanazuoni mbobevu nchini, Jenerali Ulimwengu amepewa onyo kali na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai kwa kile kilichoelezwa ni tabia yake ya kukashifu Bunge mitandaoni.

Spika Ndugai akizungumza wakati wa mjadala wa marekebisho ya sheria mbalimbali uliowasilishwa bungeni ameeleza kuwa Jenerali Ulimwengu, mwandishi nguli wa habari nchini ambaye amewahi kushika nyadhifa kadhaa za uongozi nchini ikiwemo Mkuu wa Wilaya, amekuwa akilikashfu na kulitukana Bunge apendavyo.

‘Salamu zimfikie kuwa, hili ni onyo la mwisho, asitukadirie na kutuchezea atakavyo, akirudia tutamshughulikia kwa ndani na nje hadi mahakamani, sisi sio wa kuchezewa chezewa.’ Amesisitiza Spika Ndugai

error: Content is protected !!