Ugonjwa usiojulikana waibuka nchini Congo

HomeKimataifa

Ugonjwa usiojulikana waibuka nchini Congo

Ugonjwa usiojulikana, umezuka Katika Jamhuri ya Kidemorasia ya Congo (DRC) huku ukiwaathiri watoto.

Imeelezwa kwamba karibu watoto 7,000 wako katika matibabu baada ya kuambukizwa ugonjwa huo kufuatia mlipuko (mlipuko wa ugonjwa) wake mkubwa uliotokea mwezi Agosti mwaka huu.

Dalili ni pamoja na homa kali, kutapika, maumivu makali ya tumbo na kuhara.

Imerpotiwa kwamba sampuli za ugonjwa huo zilipelekwa maabara tangu mwezi Novemba,2020 lakini mgomo wa wafanyakazi wa matibabu katika Mkoa wa Kwilu ulicheleweshwa tahadhari ya mapema.

BBC imeeleza kwamba watoto 286 wenye umri wa kati ya mwaka 0 na 5 walifariki katika kipindi cha miezi mitatu kutokana na ugonjwa ambao haukujulikana asili yake,

Kwa sasa sampuli zimefikishwa mji mkuu Kinshasa kwenye taasisi ya serkali inaoyochunguza sampuli tangu tarehe saba mwezi huu , na sasa wanaendelea kusubiri matokeo.

” Tulianza na visa zaidi ya elfu tano lakini kwa sasa tumekuwa na visa zaidi ya elfu saba tangu tarehe nane ya mwezi huu na watoto mia mbili na thamanini na sita wameshafariki.

Takwimu ni hizo hizo tu kwasasa kwabababu serkali ya jimbo ilitoa pesa na tumeeanza kutoa matibabu kwa watoto, kwa sasa tumengudua kama ni malaria lakini tukilinganisha na miaka iliyopita, kesi zinaongezeka kwa mara tano kwa hiyo tunaona ya kwamba limekuwa janga linigine jipya” amesema Mkuu wa kitengo cha afya cha jimbo la Kwilu, Dkt Jean Pierre Basele.

Serikali ya Congo imelaumiwa na baadhi ya mashirika ya kiraia nchini humo. kwa kuchelewa kutoa majibu kila mara kukiwa na milipuko ya magonjwa.

error: Content is protected !!