EAC yaongeza mwanachama mpya

HomeKimataifa

EAC yaongeza mwanachama mpya

Kikao cha Wakuu wa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wameiingiza Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) kuwa mwanachama wa jumuiya hiyo.

Katika mkutano wa 19 wa wakuu wa nchi za EAC uliofanyika kwa njia ya mtandao, Mwenyekiti wa EAC Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema ukanda wa Afrika Mashariki umeweka historia mpya kwa kukubali DRC kuwa mwanachama wa EAC, jambo litakaloongeza ushirikiano baina ya nchi hizo.

DRC inakuwa nchi ya 7 kujiunga na EAC huku wanachama wengine wakiwa ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini.

error: Content is protected !!